Lorient, Ufaransa
Beki wa zamani wa Man City, Benjamin Mendy amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Lorient ya Ufaransa ikiwa ni siku tano tangu afutiwe mashtaka ya kubaka na udhalilishaji wa kijinsia.
Mendy ambaye ni beki wa kushoto mkataba wake na Man City ulifikia ukomo hivi karibuni ingawa klabu hiyo ilimsimamisha tangu ahusishwe na tuhuma za kubaka na kudhalilisha wasichana.
Baada ya kuandamwa na kashfa hiyo akituhumiwa kwa makosa tofauti ya kubaka na kudhalilisha, Januari mwaka huu Mendy alifutiwa mashitaka sita yote yakiwa ni ya udhalilishaji kijinsia, kabla ya Ijumaa iliyopita kufutiwa mashtaka mawili ya kubaka msichana na kutaka kukaba msichana mwingine.
Mwaka 2017, Mendy alikuwa gumzo kila kona akiwa beki wa bei mbaya zaidi duniani baada ya Man City kumnunua kwa Pauni 52 milioni kutoka klabu ya Monaco ya Ufaransa.
Katika msimu wake wa kwanza aliiwezesha Man City kubeba taji la Ligi Kuu England lakini pia alikuwamo kwenye kikosi cha Ufaransa kilichobeba taji la dunia mwaka 2018 nchini Russia.
Mara ya mwisho kucheza mechi ya ushindani ilikuwa Agosti 2021 alipoiwakilisha Man City dhidi ya Tottenham lakini alikamatwa baadaye mwezi huo na kuwekwa ndani kwa miezi mitano kabla ya shauri lake kuanza kusikilizwa Agosti mwaka jana.
Mendy aliachiwa huru baada ya kukosekana ushahidi ambapo baada ya uamuzi huo mshambuliaji wa Uholanzi, Memphis Depay na Vinicius Jr wa Real Madrid walitumia mitandao ya kijamii kutoa kauli za kumtia moyo.
Kimataifa Benjamin Mendy asajiliwa Lorient
Benjamin Mendy asajiliwa Lorient
Read also
