Na mwandishi wetu
Nahodha wa Azam FC, Sospeter Bajana amesema mazoezi na mbinu wanazopewa na kocha mpya wa timu hiyo, Yossoufa Dabo zimekuwa zikiwasuka vilivyo hasa kuelekea michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Azam ambayo imejichimbia Sousse, Tunisia kwa kambi ya maandalizi ya msimu ujao tayari imeshacheza mechi moja ya kirafiki na Al Hilal, na leo wakitaraji kuikabili Esperance ya nchini humo.
“Mazoezi ni magumu, kama inavyofahamika mazoezi ya utimamu wa mwili yanahitaji uvumilivu na tumeonesha hilo, tunaomba tuendelee kuwa hivi hivi tuweze kukipata tunachokitaka kuelekea msimu ujao.
“Mazoezi yamekuwa na utofauti kidogo, walimu wapya wanasisitiza zaidi nidhamu na mbinu ambazo wanatuelekeza na sisi tupo tayari kuchukua vitu vyao vipya kwa ajili ya kufanya vizuri tuendako pia tuna michuano mikubwa iliyo mbele yetu,” alisema Bajana.
Alifafanua kuwa michezo yao ya kimataifa pia imekuwa ikiwasaidia mno kuwaweka vizuri ikizingatiwa wanakutana na timu kubwa, hivyo inawajenga vilivyo na inasaidia benchi la ufundi kufahamu mapungufu yao kwa timu kama hizo.
Soka Bajana asifia mazoezi Azam
Bajana asifia mazoezi Azam
Read also
