Oliveira, Ureno
Mchezaji anayeaminika kuwa na umri mkubwa kuliko wote duniani anayecheza soka la ushindani, Kazuyoshi Miura (pichani) mwenye miaka 56 ameongeza mkataba wa kuichezea UD Oliveirense ya Ureno huku akipanga kustaafu soka akiwa na miaka 60.
Oliveirense, kwa sasa inashiriki michuano ya Liga Portugal 2 ambayo ni ligi ya tatu kwa ukubwa nchini Ureno baada ya Primeira Liga na Liga Portugal 1.
Miura ambaye pia alikuwa mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Japan, alijiunga na Oliveirense kwa mkopo Januari mwaka huu akitokea Yokohama, ataendelea kuichezea timu hiyo kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Katika mechi ya mwisho ya msimu uliopita wa soka nchini Ureno dhidi ya Leixoes, Miura alicheza mechi hiyo na timu yake ilitoka na ushindi wa mabao 4-3 na yeye kuwa nyota wa mchezo.
Alianzia kucheza soka la ushindani nchini Brazil mwaka 1986 katika klabu ya Santos lakini amekuwa na klabu ya Yokohama FC tangu mwaka 2005.
Miura pia amewahi kucheza kwa mkopo katika klabu ya Suzuka Point Getters ambayo kocha wake ni mdogo wake Yasutoshi, katika mechi 18 alizoichezea timu hiyo, alifunga mabao mawili.
Mbali na Brazil na Japan, Miura pia amecheza soka la ushindani katika nchi za Italia, Croatia na Australia na kwa upande wa timu ya Taifa ya Japan, ameichezea timu hiyo mara 89 na kufunga mabao 55 kabla ya kustaafu kuichezea timu hiyo miaka 23 iliyopita.
Miaka ya nyuma, Miura aliwahi kuulizwa na waandishi wa habari anafikiria kustaafu soka lini, akasema kwamba mpango wake ni kustaafu akifikisha miaka 60.
Kimataifa Miura, ana miaka 56 hataki kustaafu soka
Miura, ana miaka 56 hataki kustaafu soka
Related posts
Read also
