Na mwandishi wetu
TIMU ya Azam FC imeendelea kuweka wazi usajili wake wa msimu ujao kwa kumtangaza beki wao mpya wa kushoto mwenye sifa ya kupandisha mashambulizi, Cheikh Sidibe aliyesaini mkataba wa miaka miwili.
Sidibe (pichani) ametangazwa na Azam saa chache leo Jumanne jioni baada ya kutangaza kumnasa Msenegali mwingine ambaye ni mshambuliaji, Alassane Diao kutoka US Goree ya mchini kwao.
Azam katika kurasa zake za mitandao ya kijamii wakimtambulisha Sidibe pamoja na kueleza furaha yao ya kumasa beki huyo pia walimsifia kwa kuandika: “Sidibe, 24, ni beki mahiri wa kushoto akiwa fundi wa kupandisha mashambulizi na kupiga mipira ya adhabu ndogo.”
Beki huyo aliyewahi kuitumikia Generation Foot ya Dakar amesajiliwa Azam akitokea Teungueth FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Senegal na anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na timu hiyo.
Waliomtangulia Sidibe ni Diao, kiungo mshambuliaji Mgambia, Djibril Sillah na kiungo wa kati, Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyekuwa Yanga SC.
Soka Beki Msenegali asaini Azam FC
Beki Msenegali asaini Azam FC
Read also
