London, England
Arsenal imeamua kwa mara ya tatu kuwasilisha rasmi ofa ya Pauni 105 milioni kwa ajili ya kumsajili kiungo wa West Ham na timu ya Taifa ya England, Declan Rice.
Hatua ya Arsenal ni kama inaamsha vita yake na Man City katika kumuwania kiungo huyo ambaye inadaiwa kocha wa Man City Pep Guardiola naye amemuingiza katika hesabu zake kwa ajili ya msimu ujao hasa baada ya kuondoka kwa Ilkay Gundogan.
Haijaweza hata hivyo kufahamika mara moja iwapo Man City ambao ofa yao ya Pauni 90 milioni ilikataliwa jana Jumanne kama watakuwa tayari kuongeza chochote ili wampate mchezaji huyo.
Wakati Man City na Arsenal zikiwa katika vita ya kimya kimya, Rice mwenye umri wa miaka 24, zipo habari kwamba mapenzi yake yapo zaidi Arsenal kuliko Man City ingawa kinachoonekana ni kwamba West Ham imepania kutengeneza pesa ndefu kupitia mchezaji huyo.
Rice ametokea kuwa kivutio katika kikosi cha West Ham msimu wa 2022-23, ameiwezesha timu hiyo kubeba taji la Europa Conference Ligi, lakini pia ni kati ya wachezaji wa England waliong’ara na timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia Desemba mwaka jana.
Kuhusu hatma yake, Rice ambaye mkataba wake na West Ham unafikia mwisho mwakani, amewahi kunukuliwa mara kadhaa akisema kwamba anataka kusaka changamoto mpya nje ya klabu hiyo.
Kimataifa Arsenal yampandia dau Rice
Arsenal yampandia dau Rice
Read also
