Roma, Italia
Chozi la furaha. Ndicho kilichomtokea kocha wa Roma ya Italia, Jose Mourinho baada ya timu yake kufuzu hatua ya fainali ya Europa Conference League.
Mourinho ambaye amewahi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na klabu ya FC Porto ya Ureno na Inter Milan ya Italia, Alhamisi juzi aliibwaga Leicester City katika mechi ya nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.
Katika mechi ya jana, Roma ikiwa nyumbani iliibuka na ushindi wa bao moja baada ya matokeo ya mechi ya kwanza ya nusu fainali ambayo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 na sasa inasubiri kuumana na Feyernoord katika mechi ya fainali itakayopigwa Mei 25.
Alikuwa ni Tammy Abraham aliyeipatia Roma bao ambalo lilimfanya Mourinho atokwe chozi la furaha ambako baada ya hapo alinukuliwa akisema, “Mimi ni mtu mwenye hisia (mihemko), kwetu hii ni sawa na Ligi ya Mabingwa.”
“Unapokuwa unaishi Roma, unafanya kazi Roma na kupumua ukiwa Roma, hapo unapumua hii klabu kwa sababu ama hakika ni klabu ya mji huu, nililiona hilo katika siku ya kwanza ni jambo kubwa lakini hakuna ushindi wa mara kwa mara na hakuna fainali nyingi, historia haiendani na hali halisi kwa klabu.”
“Tumeweza kuijenga timu, timu ambayo imekuwa hatua kwa hatua ili tuweze kuifunga timu ya Ligi Kuu England , ni kweli kwamba yapo matukio makubwa ya kukumbukwa kuliko hili lakini sijifikirii mimi peke yangu bali nawafikiria watu wa hapa na wachezaji wangu.”
Kimataifa Ushindi wamtoa chozi Mourinho
Ushindi wamtoa chozi Mourinho
Related posts
Read also
