Na mwandishi wetu
Klabu ya Azam FC imemuongezea mkataba wa miaka motatu kiungo wake, Sospeter Bajana (pichani) utakaomuweka katika timu hiyo hadi mwaka 2026.
Azam imeeleza juu ya hilo Jumatano hii kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuhusiana na hilo wakiandika: “Mkata umeme halisi na nahodha wetu, Sospeter Bajana ataendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2026.”
Taarifa za kuongeza mkataba kwa Bajana ambaye msimu uliopita alikuwa na msimu bora kwa kiwango alichokionesha, kunazima tetesi zilizokuwa zikizagaa kwenye duru za michezo kuwa anatarajia kutua Simba SC.
Bajana anakuwa mchezaji wa kwanza kuelezwa kuongezewa mkataba na timu hiyo kuelekea msimu ujao baada ya hivi karibuni timu hiyo kuwatema wachezaji wake sita mpaka sasa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kurekebisha kikosi chao wakijiweka tayari kwa michuano ya ndani na yale ya Afrika.
Wachezaji waliotemwa mpaka sasa ni Wilbol Maseke, Ismail Aziz, Cleophas Mkandala, Rodgers Kola, Kenneth Muguna na Bruce Kangwa.
Soka Bajana aongezewa mkataba Azam FC
Bajana aongezewa mkataba Azam FC
Read also
