Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm amesema ushindani wao na Azam wa kuwania kumaliza nafasi ya tatu umewafanya wasitishe mambo ya usajili kwa sasa hadi ligi itakapomalizika.
Singida Big ipo nafasi ya nne na pointi 54, Azam ni ya tatu kwa pointi 56 huku ikiwa imesalia mechi moja kuhitimisha Ligi Kuu NBC msimu huu.
Pluijm alisema pia wanahitaji kuimarisha timu kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao lakini kwa sasa wanatazamia kumaliza vizuri ligi kisha wageukie mchakato huo aliodai unahitaji umakini mno kulingana na michuano iliyo mbele yao msimu ujao.
“Lazima usajili ufanyike, tuboreshe timu kuelekea msimu ujao ambapo tunatarajia kuwa na michuano mingi lakini hilo kwanza lipo pembeni kwa sasa, kikubwa nahitaji kuifanikisha timu kumaliza vizuri.
“Mwisho wa msimu tukimaliza kabisa hesabu za ligi ambapo siku si nyingi tutakamilisha hilo basi nitageukia moja kwa moja kwenye mambo ya usajili, kuhakikisha tunajiweka sawa kwa msimu ujao,” alisema Pluijm.
Soka Azam yasitisha usajili Singida Big
Azam yasitisha usajili Singida Big
Read also
