London, England
Kocha wa England, Gareth Southgate ametangaza kikosi kwa ajili ya mechi za kufuzu Euro 2024 akimuacha straika wa Chelsea, Rahim Sterling (pichani) na kumwita mara ya kwanza kiungo wa Crystal Palace, Eberechi Eze
Eze ameitwa katika kikosi hicho akiwa na rekodi ya kufunga mabao sita katika Ligi Kuu England ingawa kuachwa kwa Sterling kumeacha maswali kwa baadhi ya mashabiki.
Southgate ambaye pia amemuita katika kikosi hicho beki wa kati wa Man United, Harry Maguire ambaye amekuwa na wakati mgumu msimu huu, alifikia uamuzi wa kumuacha Sterling ambaye pia ni mshambuliaji wa zamani wa Man City baada ya kufanya naye kikao na kukubaliana uamuzi huo.
Akilezea kuhusu Sterling, Southgate alisema, “haifurahii hali yake kimwili, amekuwa na matatizo ya misuli, hakuwa hasa mwenye kufikiriwa, hadhani kama anacheza katika kiwango anachokihitaji.”
England ambayo ipo Kundi C itaumana na Malta mjini Ta’ Qali mechi itakayopigwa Juni 16 kabla ya kuumana na North Maacedonia kwenye dimba la Old Trafford siku tatu baadaye.
Timu hiyo ambayo inashika usukani wa kundi hilo ikiwa tayari imeshazifunga timu za Italia na Ukraine katika mechi zake mbili za kwanza zilizopigwa Machi mwaka huu.

Kikosi kamili cha England na timu wanazotoka kwenye mabano ni kama ifuatavyo… Makipa: Sam Johnstone (Crystal Palace), Jordan Pickford (Everton), Aaron Ramsdale (Arsenal)
Mabeki: John Stones (Man City), Kieran Trippier (Newcastle), Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Lewis Dunk (Brighton), Marc Guehi (Crystal Palace), Harry Maguire (Man United), Tyrone Mings (Aston Villa), Luke Shaw (Man United) na Kyle Walker (Man City)
Viungo: Jude Bellingham (Borussia Dortmund), Eberechi Eze (Crystal Palace), Conor Gallagher (Chelsea), Jordan Henderson (Liverpool), Kalvin Phillips (Man City), Declan Rice (West Ham)
Washambuliaji: Marcus Rashford (Man United), Bukayo Saka (Arsenal), Callum Wilson (Newcastle)Phil Foden (Man City), Jack Grealish (Man City), Harry Kane (Tottenham) na James Maddison (Leicester City).
