Roma, Italia
Kocha wa AS Roma, Jose Mourinho amepuuza uvumi unaomhusisha na mipango ya kujiunga na klabu ya PSG ya Ufaransa akidai anauheshimu mkataba wake na Roma unaofikia ukomo mwaka 2024.
PSG kwa sasa inanolewa na Christophe Galtier ambaye habari zilizopo ni kwamba hatokuwa na timu hiyo msimu ujao huku Mourinho akitajwa kumrithi na tayari zipo habari kwamba mabosi PSG wamefanya mazungumo na mshauri wa kocha huyo.
Akizungumzia habari ya kuhusiswa na PSG. Mourinho mbali na kuahidi kuendelea kuuheshimu mkataba wake na AS Roma alisema, “kama walinipigia (PSG) basi hawakunipata.”
Roma leo Alhamisi itakuwa mwenyeji wa Bayer Leverkusen katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Europa Ligi.
Leverkusen kwa sasa inanolewa na Xabi Alonso, nyota wa zamani wa Real Madrid ambaye wakati akiichezea timu hiyo, Mourinho alikuwa kocha wake kati ya mwaka 2010 na 2013.
Akimzungumzia Alonso, Mourinho alieleza anavyovutiwa na nyota huyo wa zamani wa Hispania, “Sikuonana naye kwa kipindi kirefu tumekuwa vizuri kwa wakati wote, tulikuwa ni zaidi ya kocha na mchezaji,” alisema Mourinho, kocha wa zamani wa Chelsea.
Kimataifa Mourinho apuuza hadithi ya PSG
Mourinho apuuza hadithi ya PSG
Read also
