London, England
Straika wa Tottenham, Harry Kane amefikisha mabao 209 katika Ligi Kuu England (EPL) na kushika nafasi ya pili nyuma ya straika wa zamani wa Newcastle, Alan Shearer aliyefunga mabao 260.
Kane ambaye alifunga bao lake la 209 jana Jumamosi katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace, amempiku nyota wa zamani wa Man United, Wayne Rooney aliyekuwa akishikilia nafasi ya pili na mabao yake 208.
Kwa sasa Kane ana kazi ya kuifukizia rekodi ya Shearer ambaye aliwahi kunukuliwa akimtaka mchezaji huyo kupigania taji kwa kutafuta changamoto kwingineko badala ya kuwekeza nguvu katika kusaka rekodi pekee.
Rekodi ya Shearer ya mabao 260 ambayo aliiacha tangu astaafu soka la ushindani mwaka 2006 ni mlima ambao Kane ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya England, ana nia ya kuupanda.
Jambo la kufurahisha kwa Kane ni kwamba amempiku Rooney akitumia mechi 317 kufikisha mabao 208, mechi ambazo ni pungufu ya mechi 174 alizotumia Rooney kufunga mabao hayo.
Akizungumzia mafanikio ya Kane ambaye kwa sasa ana miaka 29, kocha wa zamani wa England, Roy Hodgson alisema kwamba Shearer anahitaji kuguswa na jambo hilo.
“Ni bado kijana, bado ana mengi katika soka mbele yake, nina hakika Alan (Shearer) anahitaji kuguswa na rekodi yake ya mabao kwa sababu Kane atakuwa anamfukuzia kwa karibu,” alisema Hodgson.
Kimataifa Kane aisaka rekodi ya Shearer EPL
Kane aisaka rekodi ya Shearer EPL
Read also
