Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba imepata Sh milioni 188.9 kama mgawo wa mapato ya mchezo wa ‘Derby ya Kariakoo’ dhidi ya Yanga, uliochezwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao Simba ilikuwa mwenyeji, uliingiza mashabiki 53,569, ambapo VIP A, waliingia 340 kwa kiingilio cha Sh 30,000 na kupatikana Sh milioni 10.2 na VIP B waliingia watazamaji 4,160, kwa kiingilio cha Sh 20,000 na zilipatikana Sh 83.2 milioni.
VIP C waliingia mashabiki 2,004 kwa Sh 15,000 na kupatikana Sh milioni 30.06 wakati jukwaa la rangi ya machungwa liliingiza watazamaji 10,372 waliolipa Sh 10000 na kuingiza Sh 103. 7 milioni na mzunguko waliingia watazamaji 36,693 waliolipa Sh 5,000 na kuingiza Sh 183.4 milioni.
Mchanganuo huo uliowekwa wazi leo Alhamisi na TFF kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ulionesha kuwa malipo ya VAT ni Sh 62.6 milioni, BMT walichukua Sh10.4 milioni, gharama za tiketi Sh 22.5 milioni na uwanja Sh milioni 47.2 milioni.
Gharama za mchezo ilikuwa Sh milioni 22, TFF ikichukua Sh milioni 12.5 milioni huku Bodi ya Ligi ikibeba Sh milioni 25.1 milioni na FA Mkoa ikinyakua Sh 18.8 milioni.
Mchezo uliisha kwa Yanga kufungwa mabao 2-0. Mabao ya Simba yakiwekwa kimiani na Henock Inonga na Kibu Denis.
Soka Simba yaingiza Sh 189 milioni Kariakoo Derby
Simba yaingiza Sh 189 milioni Kariakoo Derby
Read also
