London, England
Mechi za leo Jumanne za Ligi Kuu England (EPL) zitasimama kwa muda mfupi kwa lengo la kuwapa wachezaji waislam muda wa kufuturu katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan.
Utaratibu huo utafanywa kama klabu zitaomba kabla ya mechi ambapo mwamuzi atatoa ishara ya kusimamisha mchezo ili kuwapa nafasi wachezaji hao kula na kunywa pembeni ya uwanja.
Mechi ya Everton na Tottenham iliyochezwa jana Jumatatu usiku ilisimamishwa katika dakika ya 26 kwa lengo la kuwapa nafasi wachezaji waliofunga kupata chochote cha kuupa mwili nguvu.
Katika mechi hiyo wachezaji watatu wa Everton, Abdoulaye Doucoure, Amadou Onana na Idrissa Gueye walipata fursa hiyo kwa kuruhusiwa kupata mlo baada ya mwamuzi kusimamisha mechi.
Katika utaratibu huo mwamuzi hatosimamisha mchezo wakati wachezaji wakipigania mpira badala yake fursa ya aina hiyo itatolewa na mwamuzi wakati wa mpira wa kurushwa, adhabu au mpira unapotoka.
Timu husika pamoja na waamuzi watajadili suala hilo kabla ya mechi na kukubaliana muda sahihi wa kusimamisha mchezo ili wachezaji waliofunga waweze kupata chochote cha kuupa mwili nguvu.
Mechi za leo Jumanne za EPL ni kama ifuatavyo…
Bournemouth v Brighton
Leeds v Nottm Forest
Leicester v Aston Villa
Chelsea v Liverpool
Kimataifa Mechi EPL yasimama wachezaji wafuturu
Mechi EPL yasimama wachezaji wafuturu
Read also
