Na mwandishi wetu
Kiungo wa Simba, Clatous Chama ametangazwa mfungaji wa bao bora la mzunguko wa tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika huku mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele akiingia katika kinyang’anyiro cha kuwania bao bora la mzunguko wa tano wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Mayele aliyefunga bao lake la tatu msimu huu kwenye michuano hiyo ameingia kupitia bao alilofunga Jumapili iliyopita dhidi ya US Monastir waliposhinda mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Mabao mengine mawili yanayoshindanishwa ni la Ousmane Kamissoko wa Real Bamako dhidi ya TP Mazembe waliposhinda 2-0 na lingine la Mydo Nakouho wa DC Motema Pembe walipopoteza mbele ya Asec Mimosas kwa mabao 2-1.
Chama ametangazwa mshindi kupitia bao alilofunga kwa adhabu ndogo dakika ya 10 walipokuwa wakicheza na Horoya AC Jumamosi iliyopita katika ushindi wao mnono wa 7-0, Uwanja wa Mkapa.
Katika kinyang’anyiro hicho Chama ambaye amewaangusha Percy Tau wa Al Ahly, Zakaria Draoui (Zamalek), Soufiane Benjdida (Vipers) na Sadio Kanoute (Simba) kwenye bao bora, ameshindwa kwenye kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa wiki wa michuano hiyo na kutua kwa Mahmoud Kahraba wa Al Ahly.
Mbali na Kahraba na Chama wengine waliokuwa wakiwania mchezaji bora wa wiki ni Sadio Kanoute na Percy Tau. Al Ahly iliifunga Cotton mabao 4-0 wikiendi iliyopita.
Kimataifa Chama afunga bao bora Ligi ya Mabingwa
Chama afunga bao bora Ligi ya Mabingwa
Read also
