Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kuwa licha ya ubora aliokuwa nao beki wa kati wa timu hiyo, Mamadou Doumbia, bado anahitaji muda zaidi ili aweze kuzoea falsafa zake.
Doumbia (pichani kulia) ambaye amejiunga na Yanga katika dirisha dogo la usajili akitokea Stade Malien ya Mali, amepata nafasi ya kucheza mchezo mmoja wa Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Rhino Rangers ambapo aliingia akitokea benchi.
Safu ya ulinzi ya Yanga ambayo imeruhusu mabao 10 pekee kwenye Ligi Kuu NBC hadi sasa huku pacha ya Dickson Job na Yannick Bangala ikifanya kazi nzuri ya kuiweka salama ngome ya mabingwa hao watetezi.
Nabi alisema kuwa anajua kiu ya mashabiki ni kumuona beki huyo wa kati akianza kwenye michezo ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Afrika ili kuongeza uimara wa safu ya ulinzi ya timu.
“Doumbia ni mchezaji mzuri ambaye naamini anaenda kuongeza kitu kwenye kikosi changu sio rahisi kuona akianza kucheza haraka hivyo ndio maana anaendelea kupikwa taratibu kujua falsafa za timu.
“Nimeona watu wanaongelea sana kuhusu Mamadou (Doumbia), si kila mchezaji akiletwa basi ataanza kucheza kwa haraka, huyu ni beki wa kati hili ni eneo ambalo unahitaji utulivu kumuingiza mtu mpya.
“Tunafanya kazi kubwa sasa ya kumfanya Doumbia azoee, wakati wake ukifika atacheza tu akishafanikiwa kucheza kama tunavyotaka. Huyu si mshambuliaji ambaye anaweza kuja na ukampa nafasi,” alifafanua Nabi.
Soka Nabi: Doumbia anahitaji muda
Nabi: Doumbia anahitaji muda
Read also
