Paris, Ufaransa
Vigogo wa klabu za Paris Saint-Germain (PSG) na Chelsea inadaiwa walikutana Jumanne hii kujadili uhamisho wa mshambuliaji wa PSG, Neymar Jr kujiunga na Chelsea.
Habari za ndani zinadai kuwa vigogo hao ni Rais wa PSG, Nasser al Khelaifi na mmiliki mwenye hia nyingi Chelsea, Todd Boehly walikutana huku ikidaiwa kuwa PSG inataka kuachana na mchezaji huyo.
Majira ya Kiangazi mwaka jana PSG walionyesha nia ya kutaka kuachana na Neymar lakini haikuweza kupatikana klabu ya kumnunua mchezaji huyo ambaye mkataba wake PSG unafikia ukomo Juni 2027.
Neymar ambaye pia ni mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil kwa sasa ana miaka 31 na inaonekana kama ameanza kupoteza mvuto uliozoeleka katika kikosi cha vinara hao wa Ligi 1 nchini Ufaransa.
Tangu majira ya kiangazi mwaka jana Boehly inadaiwa alipewa ofa ya kumnunua Neymar lakini mpango huo ulikwama huku ikidaiwa hata aliyekuwa kocha Chelsea, Thomas Tuchel naye alipenda kumsajili mchezaji huyo.
Al Khelaifi na Boehly pia inadaiwa walijadiliana kuhusu usajili wa Hakim Ziyech ambaye PSG walitaka kumsajili akitokea Chelsea lakini kama ilivyokuwa kwa Neymar, mpango huo pia ulikwama.
Kimataifa Chelsea, PSG zamjadili Neymar
Chelsea, PSG zamjadili Neymar
Read also
