Na mwandishi wetu
Klabu ya KMC imemtangaza beki wao, Hance Masoud (pichani) kutokuwa miongoni mwa wachezaji watakaoitumikia timu hiyo kwenye mechi zilizobaki baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni.
Masoud ni kati ya nyota saba wa kikosi cha kwanza waliokuwa majeruhi lakini imeelezwa kuwa wengine wamepona na kurejea kuipambania timu hiyo kasoro beki huyo wa kushoto.
Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala ameeleza kuwa Masoud atalazimika kukaa nje kwa miezi mitatu, hivyo atakaporejea ligi itakuwa inaelekea mwishoni au imemalizika.
“Ni pigo kumkosa Masoud kwa kipindi hiki ambacho ligi inaelekea mwishoni na inazidi kuwa ngumu, upasuaji wake utamuweka nje kwa miezi mitatu, mpaka apone na arejee kuwa fiti ni kipindi kirefu zaidi hivyo tutamkosa kwa kipindi hiki kilichobaki,” alisema Mwagala.
Mwagala alisema pamoja na pigo hilo lakini wanashukuru kurejea kwa baadhi ya nyota wao wengine kama Matheo Anthony, Waziri Junior, Awesu Awesu, Daruwesh Saliboko ambao wataiongezea nguvu timu hiyo kutimiza ndoto zao za msimu huu.
Soka KMC yamuondoa beki kikosini
KMC yamuondoa beki kikosini
Read also
