Na mwandishi wetu
Winga wa Yanga, Bernard Morrison aliyeachwa na timu hiyo ikielekea nchini Tunisia kutokana na majeraha ya nyonga tayari ameanza mazoezi ya peke yake kujiweka sawa akiwa Dar es Salaam.
Mchezaji huyo raia wa Ghana ameanza mazoezi ‘gym’ leo Jumatano ili kuweka sawa nyonga yake hiyo inayomlazimu kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili.
Morrison ambaye mara ya mwisho kuitumikia Yanga ilikuwa mechi waliyoshinda mabao 3-2 dhidi ya Azam Desemba 25, mwaka jana alielezwa kuwa yuko kwao Ghana kwa ruhusa kabla ya baadaye kuelezwa ana majeraha hayo.
Rais wa klabu hiyo, Hersi Said alikaririwa akisema ingawa hakuwa na majeraha ya kumuweka nje moja kwa moja lakini imewalazimu kumuacha ili apone kabisa na aisaidie timu katika kipindi kigumu cha mwisho wa msimu.
Aidha, Yanga iliondoka jana Jumanne na imefika leo Tunisia kwa ajili ya mechi yao ya kwanza ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir itakayopigwa Februari 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Olimpiki Rades mjini Tunis.
Soka Morrison aanza kujifua
Morrison aanza kujifua
Read also
