Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Singida Big Stars, Bruno Gomes amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu NBC msimu huu huku tuzo ya kocha bora ikitua kwa kocha wa timu hiyo, Hans Pluijm.
Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu leo kwa vyombo vya habari, kikao cha Kamati ya Tuzo za TFF kilichofanyika Dar es Salaam wiki hii, kilimchagua Gomes baada ya kuonesha kiwango bora kwa mwezi huo akifunga mabao mawili katika mechi mbili zilizochezwa mwezi huo.
Singida Big iliifunga Kagera Sugar ya Kagera bao 1-0 na kupata ushindi mwingine kama huo dhidi ya Azam FC huku Gomes (pichani juu) aking’ara katika mechi hizo.
Gomes raia wa Brazil aliwashinda wachezaji Ibrahim Abdallah wa Namungo na Henock Mayala wa Polisi Tanzania alioingia nao fainali.
Kwa upande wa Pluijm, aliwashinda Roberto Oliveira wa Simba na Nasreddine Nabi wa Yanga alioingia nao fainali baada ya kuiongoza Singida Big Stars kushinda michezo miwili na kuendelea kushika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Kamati hiyo ya tuzo pia, imemchagua Meneja wa Uwanja wa Highland Estates uliopo Mbarali, Mbeya, Malule Omary kuwa meneja bora wa uwanja kwa mwezi Januari kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.
Soka Pluijm, Gomes wang’ara Januari
Pluijm, Gomes wang’ara Januari
Read also
