Liverpool, England
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema hasumbuliwi na nafasi za mabao anazopoteza Darwin Nunez katika mechi za karibuni badala yake anaifananisha hali hiyo na kilichowahi kumkuta Robert Lewandowski katika siku za mwanzo akiwa Borussia Dortmund.
Nunez aliyesajiliwa Liverpool msimu wa kiangazi hadi sasa amefunga mabao tisa kwa msimu huu ambao ni wa kwanza kwake lakini pia amepoteza nafasi kadhaa muhimu jambo ambalo tayari limeanza kuibua maswali.
Klopp hata hivyo anasema kwamba Lewandowski pia alikuwa na tatizo hilo hilo la kiwango kuyumba baada ya kusajili Dortmund mwaka 2010 akitokea Lech Poznan.
“Kuna mengi ya kufanana, niwe mkweli, nafikiri Lewy (Lewandowski) anaweza kuzungumziwa habari hiyo hiyo, tumekuwa na mazoezi ya kupiga mashuti, mazoezi ambayo hakumaliza, tumekuwa tukishindana kwa kuwekea na pesa unapiga, ukifunga zaidi ya mara 10 unalipwa Euro 10, usipofunga unanilipa mimi, mfuko wangu ulijaa pesa,” alisema Klopp.
“Ni suala la kutulia, unapoona mtu ana sifa zote, tulia,” alisema Klopp akimzungumzia Nunez ambaye alisajiliwa kwa Pauni 64 milioni kutoka Benfica na kuanza kudhihirisha thamani yake akifunga mabao saba katika mechi 10 kabla ya mapumziko kupisha fainali za Kombe la Dunia.
Hata hivyo mara baada ya kuanza kwa ligi, Nunez amekuwa akipoteza nafasi kadhaa za wazi ikiwamo katika mechi ya hivi karibuni ambayo Liverpool ilishindwa kutamba mbele ya Man City kwa kulala kwa mabao 3-2 na hali hiyo ilijitokeza katika mechi dhidi ya Aston Villa, mechi ambayo hata hivyo Liverpool ilishinda kwa mabao 3-1.
Klopp hata hivyo hana shaka kwamba mshambuliaji huyo atarudi katika ubora wake, “nafikiri wote tunakubali kwamba ni mchezaji mwenye ubora ulio wazi.”
Kimataifa Klopp: Nunez kama Lewandowski
Klopp: Nunez kama Lewandowski
Related posts
Read also
