Lusaka, Zambia
Kocha wa zamani wa klabu za Chelsea na West Ham, Avram Grant ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zambia.a,
Chama cha Soka Zambia (FAZ) kimethibitisha kwamba kocha huyo raia wa Israel amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuinoa timu hiyo.
“Nilikuwa natafuta changamoto sahihi na ndio maana nimeichagua Zambia,” alisema Grant katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo mjini Lusaka.
“Nimekuja hapa kwa sababu ya changamoto na natumaini hata wakati nitakapoondoka hapa, nitaangalia na kusema tulifanya kazi nzuri na kujenga msingi mzuri wa baadaye, nafikiri Zambia ina fursa, tumeweka malengo ambayo tunataka kuyatimiza,” alisema Grant.
Grant si jina geni katika soka la Afrika, aliwahi kuinoa Ghana na kuiongoza kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 ambapo timu hiyo ilifikia hatua ya fainali lakini ikashindwa kutamba mbele ya Ivory Coast kwa mikwaju ya penalti ingawa miaka miwili baadaye aling’atuka baada ya timu hiyo kuishia nafasi ya tatu katika mashindano hayo hayo.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 67 anachukua nafasi ya Moses Sichone ambaye amekuwa kocha wa muda tangu Septemba mwaka huu baada ya kuondoka kwa Aljosa Asanovic raia wa Croatia ingawa Sichone ataendelea na kazi yake ya awali ya kocha msaidizi.
Kimataifa Avram Grant kocha mkuu Zambia
Avram Grant kocha mkuu Zambia
Read also
