Paris, Ufaransa
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Kingsley Coman na Aurelien Tchouameni wamejikuta katika adha ya ubaguzi wa rangi kupitia mitandao ya kijamii baada ya kukosa penalti katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia.
Juzi Jumapili kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Dunia, Ufaransa ililala kwa penalti 4-2 mbele ya Argentina baada ya sare ya mabao 3-3 katika dakika 120 na hatimaye Argentina kutwaa taji la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986.
Mara tu baada ya vitendo hivyo vilivyofanywa kwenye mitandao ya kijamii, klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani anayoichezea Coman ilitoa taarifa ya kumuunga mkono mchezaji wao huyo mwenye umri wa miaka 26 kutokana na kadhia hiyo.
Penalti ya Coman iliokolewa na kipa wa Argentina, Emiliano Martinez wakati shuti alilopiga Tchouameni lilitoka nje ya lango.
“FC Bayern kwa nguvu zote inapinga kauli za kibaguzi zilizoelekezwa kwa Kingsley Coman, familia ya FC Bayern iko pamoja nawe. King, ubaguzi wa rangi hauna nafasi katika michezo na kwenye jamii yetu,” ilieleza taarifa ya klabu ya Bayern.
Shutuma za kibaguzi pia ziliwahi kutolewa kwa wachezaji wa England, Marcus Rashford, Jadon Sancho na Bukayo Saka baada ya fainali za Euro 2020 England ilipolala kwa mikwaju ya penalti 3-2 mbele ya Italia na wachezaji hao watatu wote walikosa penalti.
Kimataifa Tchouameni, Coman wabaguliwa mitandaoni
Tchouameni, Coman wabaguliwa mitandaoni
Related posts
Read also
