Na mwandishi wetu
Timu ya soka ya Geita Gold imewasili leo salama nchini Sudan kwa ajili ya mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Hilal Alsahil FC ya nchini humo.
Timu hiyo hata hivyo, imetua nchini humo bila ya mshambuliaji wake hatari, George Mpole na Saido Ntibazonkiza waliyemsajili hivi karibuni kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu za usajili wake.
Imeelezwa kuwa Mpole ameshindwa kuungana na wenzake kutokana na sababu za kutokuwa sawa kiafya japo alifanya mazoezi na kikosi hicho kilicho chini ya kocha Fred Minziro mpaka dakika za mwisho kabla ya timu hiyo kuanza safari.
“Saido na Mpole wamebaki Dar es Salaam. Saido ni masuala ya usajili ndiyo yamemkwamisha na tunasubiri mamlaka itupe maelekezo ili tumalize, George yeye alikuwa mazoezini kama kawaida lakini kwenye maandalizi ya safari alisema hajisikii vizuri kwa hiyo hakusafiri,”alisema Kivuyo.
Geita ambayo imeanza safari yake jana usiku ikipitia Addis Ababa, Ethiopia kabla ya kutua Sudan kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Mji wa Khartoum imeondoka na kikosi cha wachezaji 25.
Mechi ya kwanza ya Geita inatarajiwa kupigwa keshokutwa Jumapili kabla ya kurejea nyumbani ikiwasubiri wapinzani wao na kumenyana nao kwenye mechi ya marudiano itakayopigwa Septemba 17, mwaka huu.
Soka Geita Gold yatua Sudan bila Mpole
Geita Gold yatua Sudan bila Mpole
Read also
