Paris, Ufaransa
Dalili za msimu wa neema zimeanza kujionyesha kwa mshambuliaji wa PSG, Neymar ambaye amefunga mabao mawili Jumapili hii wakati timu yake ikiichapa Nantes mabao 4-0 katika mechi ya kuwania taji la Des Champions ambalo ni sawa na Ngao ya Jamii kwa Ligi Kuu ya NBC Bara.
Des Champions ni sawa na mechi inayoashiria kuanza kwa msimu, ni kama ilivyo kwa Ngao ya Jamii katika Ligi Kuu England ambayo mechi yake ilichezwa juzi na Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Man City.
Neymar ambaye hivi karibuni amenukuliwa akisema kwamba haijui hatma yake ndani ya PSG bila shaka kwa sasa atakuwa na amani na uhakika kwa msimu wa 2022/23 akiwa chini ya kocha mpya wa timu hiyo, Christophe Galtier aliyechukua nafasi ya Mauricio Pochettino.
Neymar alianza kwa kumuunganishia Messi pasi murua ambayo Messi aliitumia kuipatia PSG bao la kwanza kabla ya Neymar kufunga la pili kwa mpira wa adhabu wakati bao la tatu lilifungwa na Sergio Ramos kwa kisigino na la nne Neymar alilifunga kwa penalti baada ya kuchezewa rafu na Jean-Charles Castelletto akiwa eneo la hatari na mwamuzi kumpa Castelletto kadi nyekundu hapo hapo.
Kwa ushindi huo PSG sasa wanakuwa wameweka rekodi ya kulitwaa taji la Des Champions mara tisa kati ya 10 zilizopita
Ni wazi kwamba mafanikio hayo yanakuwa mwanzo mzuri kwa Neymar ambaye tayari alianza kuhusishwa na mipango ya kuondoka katika timu hiyo huku Man City iliyotajwa awali ikitangaza kutomtaka mchezaji huyo.
Kimataifa Neymar auanza msimu kwa neema
Neymar auanza msimu kwa neema
Read also
