Manchester, England
Katika mkakati wa kuiimarisha safu yake ya ushambuliaji, kocha wa Man United, Erik ten Hag amemteua mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Benni McCarthy katika jopo la makocha wa kumsaidia.
McCarthy, ambaye anatajwa kuwa ni shabiki wa Man United, amewahi kucheza katika Ligi Kuu England akiwa na timu za Blackburn Rovers na West Ham United lakini pia amewahi kuzichezea timu za Seven Stars, Ajax, Celta Vigo, Porto na Orlando Pirates.
Kati ya mafanikio anayojivunia ni kutwaa taji la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2004 akiwa na Porto wakati timu hiyo ya Ureno ikinolewa na Jose Mourinho ambapo anakumbukwa kwa kufunga mara mbili na kuitoa Man United katika hatua ya 16 bora kwenye michuano hiyo.
Wakati anaichezea timu ya Afrika Kusini au Bafana Bafana, McCarthy ameifungia timu hiyo mabao 31 katika mechi 79 kuanzia mwaka 1997 hadi 2012 na ndiye mchezaji anayeshika rekodi ya kuifungia mabao mengi timu hiyo.
Katika miaka ya karibuni, McCarthy alikuwa akiinoa timu ya Amazulu ya Afrika Kusini hapo hapo kukawa na habari kwamba alikataa ofa ya kuinoa Bafana Bafana.
Kimataifa McCarthy apewa shavu Man United
McCarthy apewa shavu Man United
Related posts
Read also
