Birmingham, England
Nyota ya mwanariadha wa Tanzania, Felix Simbu leo mchana imeng’ara katika Michezo ya Jumuiya ya Madola inayoendelea katika jiji la Birmingham baada ya kunyakua medali ya fedha katika mbio za marathon.
Simbu alikuwa akichuana na mwanariadha wa Uganda, Victor Kiplangat ambaye ndiye aliyeibuka kinara na kubeba medali ya dhahabu akitumia muda wa 2:10: 55 wakati Simbu alimaliza kwa muda wa 2:12: 29 Kiplangat anakuwa mwanariadha wa kwanza wa Uganda kushinda medali ya dhahabu katika marathon kwenye Michezo ya Madola.
Katika kinyang’anyiro hicho nafasi ya tatu ilikwenda kwa mwanariadha wa Kenya, Michael Githae ambaye alichukua medali ya shaba akitumia muda wa 2:13:16 na hivyo kukamilisha rekodi ya tatu bora katika mbio hizo kwa wanariadha kutoka nchi tatu majirani za Afrika Mashariki.
Wanariadha hao watatu kwa muda mrefu walionekana kuchuana kila mmoja akionyesha dalili za kubeba dhahabu lakini baadaye ikawa ni ushindani wa Kiplangat na Simbu kabla Kiplangat hajamuacha Simbu na kuibuka kinara.
Wakati Simba akijivunia medali hiyo, mambo hayakuwa mazuri kwa Mtanzania mwenzake, Hamis Athuman ambaye alishika nafasi ya nane.
Simbu atwaa medali Michezo ya Madola
Related posts
Read also
