Na mwandishi wetu
Kiungo mpya wa Ihefu FC, Papy Tshishimbi ameahidi kufanya mambo makubwa msimu ujao ikiwemo kuipa timu hiyo moja ya nafasi za juu kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu ujao.
Mchezaji huyo aliyewahi kutamba akiwa na mabingwa watetezi Yanga, ameeleza kuwa pamoja na ugumu uliopo lakini haoni kikwazo kitakachomzuia kutamba kutokana na uzoefu aliokuwa nao kwenye ligi hiyo.
“Najua kwamba ligi ya Tanzania kuanzia msimu uliopita imekuwa na ushindani mkubwa lakini kwangu nimejipanga kuhakikisha napambana nao na kuisaidia timu yangu mpya kufanya vizuri ikiwemo kumaliza nafasi mbili za juu,” alisema Tshisimbi.
Kiungo huyo raia wa DR Congo amefafanua kuwa ameamua kurudi kucheza Tanzania kutokana na ubora wa ligi iliyokuwa nayo ikilinganisha na ya kwao Congo lakini pia ni ligi ambayo inalipa vizuri katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Alisema anaamini Ihefu ni timu sahihi ambayo itarudisha jina lake na kumfanya awe bora kama ilivyokuwa wakati anatua kwa mara ya kwanza Yanga mwaka 2018 akitokea Mbabane Swallows ya Botswana.
Tshishimbi amejiunga na Ihefu kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Kitayose FC ya Tabora inayoshiriki Ligi ya Championship.
Soka Tshishimbi atamba kuibeba Ihefu FC
Tshishimbi atamba kuibeba Ihefu FC
Read also
