Na mwandishi wetu
Yanga imeendeleza kwa vitendo dhamira yake ya kulitetea taji la Ligi Kuu NBC msimu huu wa 2025-26 baada ya kuvuka mtihani uliotajwa kuwa mgumu kwa kuinyuka Mashujaa FC mabao 2-0.
Ushindi huo uliopatikana Jumamosi Juni 13, 2026 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma umeifanya Yanga kujiimarisha kileleni mwa wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 63 katika mechi 26.
Yanga walianza kuzitikisa nyavu za Mashujaa katika dakika ya 27 kwa bao lililofungwa na Mudathir Yahya, baada ya kuinasa pasi ya Prince Dube.
Bao hilo ni kama lilikuwa jibu kwa kocha wa Mashujaa, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye kabla ya mechi hiyo alinukuliwa akisema kuwa Mudathir ni mchezaji mjanja mjanja tu.
Hali hata hivyo ilikuwa tofauti uwanjani kwani Mudathir huyo huyo, kwa umahiri mkubwa alipokea pasi akaituliza vizuri na kwa kujiamini kabla ya kufumua shuti la juu hadi wavuni.
Kama kawaida yake Mudathir baada ya bao hilo hakuacha utaratibu wake uliozoeleka wa kujifanya anazungumza na simu akitumia ‘kilinda ugoko’ kuwa mfano wa simu ya mkononi.
Yanga waliendelea kutawala mchezo huku Mashujaa nao wakipambana kutengeneza mashambulizi kwa nia ya kupata bao la kusawazisha lakini hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo moja.
Ushindi wa Yanga ulikamilika dakika ya 90 kwa bao lililofungwa na nahodha na beki wa kati wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto.
Kimataifa Mashujaa si lolote kwa Yanga
Mashujaa si lolote kwa Yanga
Related posts
Read also
