Rabat, Morocco
Kikosi bora cha wachezaji 11 maarufu Best Eleven cha fainali za Kombe la Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 (Afcon-17) kimetajwa ambapo timu ya Tanzania, Serengeti Boys imetoa wachezaji wanne.
Serengeti Boys imeweka rekodi kwa kufikia kwa mara ya kwanza hatua ya fainali kabla ya kulala mbele ya Senegal waliobeba taji hilo kwa ushindi wa penalti 4-2 baada ya sare ya bao 1-1.
Timu hiyo iliweza kuonesha ubabe hatua ya robo fainali kwa kuitoa Algeria kabla ya kumalizia kwa kuitoa Misri katika nusu fainali na kuikabili Senegal katika fainali iliyopigwa Jumanne, Juni 2, 2026 kwenye Uwanja wa Moulay El Hassan mjini Rabat.
Wachezaji wanne wa Serengeti Boys waliomo katika Best Eleven au Best XI hiyo ni beki Hussein Mbegu na viungo Issa Chole na Dismas Athanas pamoja na winga Razak Mbegelendi.
Serengeti ambao pia wametwaa tuzo ya Fair Play, wachezaji wake mbali na kuingia katika Best XI, pia walitwaa tuzo akiwamo Chole aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora wa fainali hizo.
Mchezaji mwingine ambaye pia yumo katika Best XI ni Athanas ambaye pia ndiye aliyetwaa tuzo ya mfungaji bora au Golden Boot akibebwa na mabao yake matatu.
Kikosi kamili cha wachezaji waliomo katika Best XI ya Afcon-17 na nchi wanazotoka katika mabano ni kama ifuatavyo…
Kipa
Thierno Sow (Senegal)
Mabeki
Thierno Sow (Senegal)
Hussein Mbegu (Tanzania)
Adam Soudi (Morocco)
Lamine Mbengue (Senegal)
Viungo
Issa Chole (Tanzania)
Ahmed Abdelhalim (Egypt)
Dismas Athanasi (Tanzania)
Washambuliaji
Razaki Mbegelendi (Tanzania)
Mohamed Amine Moustache (Morocco)
Mouhamed Wagne (Senegal)
Kimataifa Serengeti Boys yatoa wanne Best Eleven Afcon-17
Serengeti Boys yatoa wanne Best Eleven Afcon-17
Read also
