Madrid, Hispania
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi wa rais wa klabu ya Real Madrid, rais wa sasa wa klabu hiyo, Florentino Pérez (pichani) ameahidi kutangaza jina kubwa la kwanza la mchezaji kwa ajili ya usajili wa msimu ujao.
Wanachama wa klabu ya Real Madrid, Jumapili, Juni 7, 2026 watapiga kura kumchagua rais katika uchaguzi wa kwanza katika kipindi cha miaka 20 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali.
Perez, 79 ,ambaye ni jina kubwa katika klabu hiyo anatarajia kupata upinzani kutoka kwa mfanyabiashara wa nishati jadidifu, Enrique Riquelme, 37.
Zipo habari kwamba Real Madrid ipo katika hatua nzuri za kumsajili beki Ibrahima Conte ambaye ameachana na klabu ya Liverpool na sasa ni mchezaji huru na huenda hilo likawa jina la kwanza kubwa katika usajili anaoutaja Perez.
Riquelme katika kampeni zake ameahidi akichaguliwa, mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Raúl González atakuwa mkurugenzi wake wa michezo na anaamini kiungo wa Man City, Rodri ni aina ya mchezaji anayetakiwa kuichezea Real Madrid.
“Alhamisi hii nitatangza jina kubwa la usajili wa msimu ujao, kila mmoja anafahamu mipango yangu katika michezo, ni kusajili wachezaji bora na kuendeleza ushindi,” alisema Perez.
Kuhusu Jose Mourinho kuwa kocha mpya wa timu hiyo, Perez hakuwa tayari kumtaja kocha huyo badsala yake alisema kwamba hivi karibuni atatangaza nani kocha mpya Real Madrid.
Kimataifa Pérez kutangaza usajili mkubwa Real Madrid
Pérez kutangaza usajili mkubwa Real Madrid
Related posts
Read also
