Na mwandishi wetu
Waamuzi kutoka Morocco ndio watakaochezesha mechi baina ya mahasimu wa jadi nchini Tanzania, Yanga na Simba itakayopigwa Jumapili Mei 3, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamhuyo jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyopatikana kwenye chanzo kimoja cha habari cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliwataja waamuzi hao kuwa ni Hamza El Fareq (pichani) ambaye ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo El Fareq atasaidiwa na waamuzi wengine kutoka Morocco ambao ni Lahsen Agaou mwamuzi msaidizi namba moja na Hamza Masiri, msaidizi namba mbili na Mustapha Kechaf ni mwamuzi wa akiba.
Hii si mara ya kwanza kwa mechi baina ya timu hizo mahasimu kuchezeshwa na waamuzi kutoka nje ya Tanzania, Juni 25 mwaka jana, mechi ya ligi baina ya timu hizo ilichezeshwa na waamuzi kutoka nchini Misri.
Waamuzi hao ni Amin Mohammed Omar aliyekuwa mwamuzi wa kati ambaye alisaidiwa na Mahmoud Ahmed mwamuzi msaidizi namba moja na Samir Gamal msaidizi namba mbili ambao wote ni kutoka Misri.
Hatua ya TFF kutumia waamuzi kutoka nje ya Tanzania katika mechi za timu hizo mahasimu inatokana na malalamiko ya mara kwa mara kuhusu hofu ya upendeleo kwa waamuzi wa ndani.
Kimataifa Waamuzi wa Morocco kuzihukumu Yanga, Simba
Waamuzi wa Morocco kuzihukumu Yanga, Simba
Read also
