Manchester, England
Kocha wa Man United, Michael Carrick amekataa kufuta uwezekano wa kurejea kwa mshambuliaji wa timu hiyo, Marcus Rashdord ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Barcelona.
Kauli ya kocha huyo wa muda imekuja wakati huu kukiwa na hali isiyoeleweka kuhusu mambo ya baadaye ya Rashford katika kikosi cha Barcelona.
Rashford, 28, ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya England mara ya mwisho kuichezea Man United, ilikuwa Desemba 2024 na kumalizia msimu uliopita akiwa Aston Villa kwa mkopo kabla ya kuhamia Barcelona katika msimu wa 2025-26.
Barcelona au Barca inaweza kumsajili Rashford kwa dau la Pauni 30 milioni wakati wa majira ya kiangazi kama sehemu ya makubaliano ambayo yatamfanya mshambuliaji huyo kubaki katika klabu hiyo.
Wakati huo huo Man United wanafuatilia kwa karibu habari za nchini Hispania zinazodai kwamba Barcelona wana nia ya kufanya mazungumzo mapya kuhusu mchezaji huyo ikiwamo kupunguza ada yake ili aendelee kuwa hapo kwa mkopo katika makubaliano mengine.
Kwa upande mwingine mabosi wa Man United wanadaiwa kutokuwa tayari kwa mazungumzo mengine kuhusu usajili wa mshambulijai huyo na badala yake wanataka kumrudisha katika klabu hiyo iwapo Barca hawatapanda dau.
Man United wanaamini kiwango cha Rashford katika La Liga kimekuwa juu hivyo wanaweza kuwa na nafasi ya kufanya mazungumzo na klabu nyingine ikiwamo kupandisha ada ya uhamisho iwapo Barca hawatakuwa tayari.
Kimataifa Carrick ampigia hesabu Rashford
Carrick ampigia hesabu Rashford
Read also
