Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Tafa Stars imeanza vibaya mechi maalum za Fifa (Fifa Series) kwa kupigwa bao 1-0 na timu ya Liechtenstein, mechi iliyochezwa Alhamisi Machi 26, 2026 kwenye Uwanja wa Pele mjini Kigali, Rwanda.
Bao pekee lililoizamisha Stars lilifungwa katika dakika ya 54 na Ferhat Saglam aliyemalizia kwa kuujaza wavuni mpira ulioanzia kwa Nicolas Hasler baada ya Liechtenstein kucheza pasi kadhaa langoni mwa Stars.
Kuingia kwa bao hilo hakukuwakatisha tamaa wachezaji wa Stars ambao kwa muda mrefu walionesha uhai wakitengeneza nafasi kadhaa ingawa tatizo la umaliziaji lilijidhihirisha katika mashambulizi hayo.
Mashambulizi ya Stars ambayo mengi yalitokea kwa mawinga pia yalikutana na kizingiti kwenye safu ya ulinzi ya Liechtenstein ambayo ilikuwa macho kudhibiti kila hatari iliyoelekezwa kwenye lango lao.
Baada ya matokeo hayo, Stars sasa inasubiri kuumana na Macau, mechi itakayochezwa Jumapili Machi 29 kwenye uwanja huo huo, mechi ambayo itatoa mshindi wa tatu wakati mechi ya fainali pia itapigwa siku hiyo hiyo kwa mechi kati ya Liechtenstein na Aruba.
Kimataifa Stars yakwama Fifa Series
Stars yakwama Fifa Series
Read also
