Manchester, England
Kocha wa Man City, Pep Guardiola amesema kuwa changamoto kubwa katika kazi yake ya ukocha ni timu ya Liverpool iliyokuwa chini ya koha Jurgen Klopp na si Real Madrid.
Pep ametoa kauli hiyo baada ya timu yake kutolewa kwa kipigo cha jumla cha mabao 5-1 baada ya kushindwa kutamba katika mechi mbili za hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Shujaa wa Real Madrid alikuwa VinÃcius Júnior aliyefunga mabao mawili katika mechi ya pili iliyopigwa jijini Manchester na Real Madrid kutoka na ushindi wa 2-1, hiyo ni baada ya Federico Valverde kuifunga Man City mabao matatu au hat trick katika mechi ya awali ambayo Real Madrid ilishinda kwa mabao 3-0.
Akizungumza baada ya mechi ya pili waliyofungwa mabao 2-1, Pep alikana hoja kwamba Real Madrid ni timu ambayo imekuwa ikiwapa changamoto kubwa badala yake alisema changamoto kubwa aliipata kwa Liverpool ya Klopp.
“Hapana kwangu changamoto kubwa nilikuwa naipata kwa Klopp na timu yake ya Liverpool,” alisema Pep ambaye pia amewahi kuzinoa timu za Bayern Munich na Barcelona.
Akizungumzia kutolewa kwa timu yake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Pep alisema limekuwa funzo kubwa kwa klabu hiyo kwa kuwa kwa miaka 12 au 13 iliyopita haikuwahi kuwa katika mashindano ya Ulaya.
“Kucheza mara nyingi dhidi ya Real Madrid na kizazi tulichonacho tumefanya jambo kubwa, wameshinda, nasi tumeshinda, wametutoa mara nyingi kuliko tulivyowatoa sisi lakini waliona jinsi tulivyocheza,” alisema.
