Na mwandishi wetu
Kocha wa timu ya Simba, Steve Barker au Steve B ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi Februari wakati mshambuliaji wa Yanga, Laurindo Dilson ‘Depu’ ametwaa tuzo hiyo kwa upande wa mchezaji bora..
Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyopatikana Jumatatu Machi 16, 2026, Depu ametwaa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao mawili katika mechi mbili na kuiwezesha Yanga kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Katika tuzo hiyo, Depu alikuwa akishindana na Idd Suleiman ‘Nado’ wa Azam FC na Rushine de Reuck wa Simba lakini kamati ya tuzo ikamtangaza Depu kuwa ndiye mshindi.
Kwa upande wa Steve alikuwa akiwania tuzo hiyo na Pedro Concalves wa Yanga na Florent Ibenge wa Azam lakini ushindi wa mechi mbili na sare moja vilitosha kuishawishi kamati kumpa ushindi Steve.
Naye Said Mpuche ambaye ni meneja wa Uwanja wa Isamuhyo amechaguliwa kuwa meneja bora wa uwanja kwa mwezi Februari kwa kufanya vizuri katika miundombinu ya uwanja na katika menejimenti ya matukio uwanjani.
Katika Ligi ya NBC Championship, Ramadhan Karanje wa B19 amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari wa ligi hiyo baada ya kufunga mabao manne katika mechi tano na kuwashinda Obrey Chirwa wa Kagera Sugar na Tariq Seif wa Polisi Tanzania.
Kwa upande wa makocha kwenye ligi hiyo hiyo, Mbwana Makata wa Polisi Tanzania ametwaa tuzo hiyo baada ya kuiwezesha timu yake kushinda mechi nne na kutoa sare moja akiwashinda Juma Kaseja wa Kagera Sugar na Zubeir Katwila wa Geita Gold.
Mabao bora katika kipindi cha mwezi Februari kwa mujibu wa kamati ya tuzo yamefungwa na Mathew Tegisi (dk ya 89) katika mechi kati ya Pamba na Coatal Union, Shekhan Ibrahim (DK 89) mechi kati ya Yanga na JKT Tanzania na Ismail Mhesa (dk 86) mechi kati ya Mtibwa na Prisons.
Kimataifa Kocha Simba atwaa tuzo Februari
Kocha Simba atwaa tuzo Februari
Read also
