Na mwandishi wetu
Vinara wa Ligi Kuu NBC, Yanga wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Azam FC katika mechi ya ligi hiyo iliyochezwa Jumapili Machi 15, 2026 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yameifanya Yanga kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 36 wakati Azam nao wamechupa hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 28.
Ikiwatumia washambuliaji wake mahiri Depu na Prince Dube, Yanga ilipata wakati mgumu kuipenya safu ya ulinzi ya Azam iliyoongozwa na kipa mkongwe Aishi Manula.
Katika harakati za kusaka mbinu za kuipenya ngome ya Azam, Yanga ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Mudathir Yahya na nafasi yake kuingia kiungo fundi, Pacome Zouzoua ambaye alikuwa majeruhi kwa muda mrefu lakini mabadiliko hayo hayakuzaa bao.
Baada ya matokeo hayo mjadala umeanza kuibuka kuhusu Yanga ikionekana kama imeanza kupoteza makali yake hasa baada ya kutoka sare kama hiyo na mahasimu wao Simba na baadaye kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Prisons.
Mjadala huo hata hivyo hauwezi kufuta ukweli kwamba timu hiyo inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya Azam inayoshika nafasi ya pili baada ya kila timu kucheza mechi 14.
Kimataifa Yanga, Azam zashindwa kufungana
Yanga, Azam zashindwa kufungana
Related posts
Read also
