Na mwandishi wetu
Baada ya sare mbili za bila kufungana dhidi ya Yanga na Dodoma Jiji, Simba imefufua upya matumaini ya kulisaka taji la Ligi Kuu NBC msimu huu wa 2025-26 baada ya kuichapa Singida Black Stars mabao 2-1.
Ushindi huo uliopatikana Jumatano Machi 11, 2026 kwenye Uwanja wa Airtel umeifanya Simba kufikisha pointi 27 ikitulia nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 12 wakiwa wamezidiwa na vinara wa ligi hiyo, Yanga kwa tofauti ya pointi tano.
Simba walianza kuzichana nyavu za Singida BS katika dakika ya saba ya mchezo huo kwa bao lililofungwa na Anicet Oura aliyefunga baada ya kuinasa pasi ya Alassane Kante.
Singida BS walifanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 37 mfungaji akiwa ni Mossi Ndumumwe akimalizia pasi aliyounganishiwa na Lamine Jarjou.
Dakika sita kabla ya kutimia dakika 90, Elly Mpanzu aliihakiksihai Simba pointi tatu muhimu kwa kuiandikia Simba bao la pili na la ushindi akiitumia vizuri pasi ya Clatous Chama.
Matokeo hayo yanazidi kuiweka Singida BS pagumu katika ligi hiyo kwani katika mechi 13 ilizocheza hadi sasa imeambulia pointi 19 na inashika nafasi ya 10.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Azam FC ikiwa ugenini ilitoka kidedea mbele ya Dodoma jiji kwa kuilaza mabao 3-0 wakati Namungo ikiwa ugenini Karatu ilichapwa mabao 2-0 na TRA United.
Kimataifa Simba yailaza Singida Black 2-1
Simba yailaza Singida Black 2-1
Read also
