Na mwandishi wetu
Mwamuzi Nassoro Mwinchui wa Tanga ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati katika mechi ya Ligi Kuu NBC kati ya watani wa jadi nchini Tanzania, Simba na Yanga itakayopigwa Machi Mosi, 2026 kwenye dimba la New Amaan, Zanzibar.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyopatikana Februari 27, 2026 ilielezxa kuwa mwamuzi huyo atasaidiwa na Kassim Mpanga wa Dar es Salaam ambaye atakuwa mwamuzi msaidizi namba moja na Hamdan Said wa Dodoma ambaye atakuwa mwamuzi msaidizi namba mbili.
Sambamba na waamuzi hao, mwamuzi wa akiba atakuwa Ramadhan Kayoko wa Dar es Salaam na mthamini waamuzi katika mechi hiyo atakuwa Israel Mjuni pia wa Dar es Salaam.
Uteuzi wa Mwinchui kuwa mwamuzi wa kati umekuja wakati presha ya mechi hiyo ikiwa juu miongoni mwa mashabiki wa klabu hizo ambapo wapo wanaohoji kama ataweza kukabiliana na presha za mechi hiyo kubwa.
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana Juni 25, 2025 katika mechi ya ligi hiyo, Yanga ilitoka na ushindi wa mabao 2-0 na mechi hiyo ilichezeshwa na mwamuzi wa kati Amin Mohammed Omar kutoka nchini Misri.
Mwamuzi huyo wa kimataifa alipewa jukumu hilo baada ya kuibuka mzozo wa muda mrefu kuhusu mechi hiyo ambayo iliahirishwa mara kadhaa hadi viongozi wa serikali kuingilia kati na hatimaye makubaliano yakafikiwa.
Soka Mwinchui kuzihukumu Simba, Yanga
Mwinchui kuzihukumu Simba, Yanga
Read also
