Na mwandishi wetu
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) itafanya kikao chake jijini Dar es Salaam, Tanzania Ijumaa Machi 14, mwaka huu chini ya rais wa shirikisho hilo, Dr Patrice Motsepe.
Baada ya kikao hicho ufanyika mkutano wa waandishi wa habari ambao pia utaoneshwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari.
Motsepe amejipatia mafanikio tangu kuchaguliwa kwake kuliongoza shirikisho hilo na hivi karibuni uongozi wake ulitangaza kuyafuta mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani yaani CHAN.
Katika kikao cha kamati ya utendaji ya CAF jijini Dar es Salaam, mambo mbalimbali yanatarajia kujadiliwa ikiwamo maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2027 ambayo yatafanyika katika nchi majirani Afrika Mashariki za Kenya, Tanzania na Uganda.
Nchi hizo kwa sasa zipo katika maandalizi ya michuano hiyo na moja ya mambo ambayo yanafanyika kwa kasi na bidii kubwa ni ujenzi wa viwanja vyenye hadhi.
Fainali za mwisho za Afcon zimefanyika nchini Morocco kuanzia mwishoni mwa mwaka 2025 kwa mafanikio makubwa na Senegal kuibuka kinara baada ya kuwabwaga wenyeji Morocco katika mechi ya fainali.
Kimataifa Vigogo CAF kukutana Dar
Vigogo CAF kukutana Dar
Read also
