Na mwandishi wetu
Jumapili ya Januari 26, 2026 imekuwa siku nzuri kwa Azam FC na Singida Black Stars, kila moja imetoka na ushindi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam ikiilaza Nairobi United na Singida ikiichapa Otôho.
Azam wakiwa ugenini waliichapa Nairobi United mabao 2-1 wakati Singida wakiwa nyumbani waliichapa Otoho ya Congo Brazzavile bao 1-0.
Azam waliokuwa ugenini Nairobi, Kenya waliianza vibaya mechi hiyo kwa kuchapwa bao la dakika ya 13 lililofungwa na Dancan Omala akiitumia vizuri pasi ya Michael Karamor.
Iliwachukua dakika nne wawakilishi hao wa Tanzania kusawazisha bao hilo kupitia kwa Jephte Kitambala ambaye alifumua shuti baada ya kuinasa pasi ya Yoro Diaby.
Timu hizo ziliendelea kupambana kila moja ikisaka bao la kuongoza lakini walikuwa ni Azam waliopata bao la ushindi dakika ya 78, bao lililotokana na shuti la Himid Mao na mpira kugonga mwamba kabla ya kumgonga kipa wa Nairobi United, Ernest Mohamed kabla ya kujaa wavuni.
Nao Singida walineemeka kwa bao pekee la Elvis Rupia na kutoka kifua mbele kwa ushindi huo mwembamba ambao ulitosha kuwatoa Otoho vichwa chini.
Kimataifa Azam, Singida mambo mazuri
Azam, Singida mambo mazuri
Read also
