Manchester, England
Klabu ya Manchester United imeeleza kuwa kiungo wake Mbrazil, Casemiro ataachana na klabu hiyo mara baada ya mkataba wake kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu wa 2025-26.
Casemiro, 33, alijiunga na Man United mwaka 2022 kwa ada ya Pauni 70 milioni akitokea klabu ya Real Madrid ya Hispania na hadi sasa ameichezea timu hiyo ya England mara 146.
Kiungo huyo ambaye pia amekuwa akiichezea timu ya taifa ya Brazil, akizungumzia mpango huo alisema kwamba anajivunia kuichezea Man United akisema ataendelea kuikumbuka kwa wakati wote.
“Nitaendelea kuwa na Man United katika maisha yangu yote, huu si wakati wa kusema kwaheri, kwa wakati huu bado kuna mengi ya kutengeneza kumbukumbu nzuri katika kipindi cha miezi minne ijayo,” alisema Casemiro.
Casemiro alisema kwa sasa bado wana wakati wa kupambania mambo mengi pamoja na ataendelea kuwa makini kwa asilimia zote kama ilivyo kawaida yake na kujitoa kwa kila kitu kwa ajlli ya mafanikio ya timu.
“Tuna mengi ya kupambania pamoja, bado kuna muda wa kujitolea kwa hali na mali ili kuisaidia klabu yetu kupata mafanikio,” alisema Casemiro.
