Rabat, Morocco
Baada ya mpambano na dakika 120 za kukata na shoka, hatimaye timu ya taifa ya Sernegal imeibuka kinara wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 baada ya kuwanyuka wenyeji Morocco bao 1-0.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili Januari 18, 2026, hadi kupata ushindi, Senegal walijikuta katika wakati mgumu wa kususia mchezo wakidai mwamuzi alikuwa akiwabeba wenyeji Morocco ingawa baadaye walirudi uwanjani kuendelea na mchezo.
Tukio hilo lilitokea katika dakika za nyongeza (dakika ya 98) kabla ya dakika 90 za kawaida kumalizika baada ya Morocco kupewa penalti iliyotokana na kosa la El Hadji Malick Diouf kumuangusha Brahim Diaz.
Wachezaji wa Senegal kwa ushawishi wa kocha wao, Pape Thiaw waliingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakisusia penalti ambayo hata hivyo Diaz, mpira alioupiga uliokolewa na kipa wa Senegal, Edouard Mendy.
Baadaye Mendy na Sadio Mane walionekana wakiwashawishi wachezaji hao kurudi uwanjani kuendelea na mchezo wakati huo timu zikiwa hazijafungana na ndipo zilipoongezwa dakika nyingine 30.
Senegal au Simba wa Teranga walizitumia vyema dakika 30 za nyongeza kupata bao dakika ya tatu (93) kwa mpira ulioanzia kwa pasi ya kisigino ya Mane aliyemuunganishia Idrissa Gana Gueye naye kumpasia Pape Gueye aliyeujaza wavuni.
Gueye licha ya kufunga bao hilo, pia ametangazwa kuwa nyota wa mchezo na baada ya mechi hiyo alisema kwamba
anajisikia furaha kupata ushindi katika mechi iliyotawaliwa na utata lakini walitulia hasa baada ya Morocco kukosa penalti.
Mane, nyota wa zamani wa Liverpool na Bayern Munich ambaye inaelezwa kuwa hizi ni fainali zake za mwisho za Afcon, akiwa ndiye nahodha katika mchezo huo alionesha ujasiri wa kuwatuliza wenzake na hatimaye juhudi zake zikazaa matunda kwa Senegal kubeba taji.
Kimataifa Senegal mabingwa Afcon 2025
Senegal mabingwa Afcon 2025
Read also
