Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangza kufunguliwa kwa pazia la usajili wa wachezaji kuanzia Januari Mosi 2026, zoezi ambalo litafungwa rasmi Januari 30, 2026.
Taarifa ya TFF iliyopatikana Alhamisi, Januari Mosi, 2026 ilieleza kuwa usajili huo wa wachezaji utazihusu timu za Ligi Kuu NBC, NBC Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake kwa msimu wa 2025-26.
Katika taarifa hiyo iliyosainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo, Klabu husika zimekumbushwa kufanya usajili kupitia mfumo wa usajili wa Fifa Connect.
TFF imezikumbusha klabu katika taarifa hiyo kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe husika na hivyo ni muhimu kuzingatia muda.
Wakati TFF ikitangaza taarifa hiyo tayari baadhi ya klabu hasa za Ligi Kuu NBC zimeanza kuhusishwa na wachezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
Mmoja wa wachezaji ambaye jina lake limeibuka katika siku za karibuni akihusishwa na timu ya Yanga ni Allan Okelo, nyota wa Uganda Cranes aliyekosa penalti katika mechi ya Afcon dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.
Soka Usajili ligi kuu mwisho Januari 30
Usajili ligi kuu mwisho Januari 30
Read also
