Madrid, Hispania
Habari ya winga wa Real Madrid, Rodrygo kutaka kuachana na timu hiyo imeibuka kwa mara nyingine na tayari timu za Arsenal, Man United na Liverpool zimeonesha nia ya kuitaka huduma ya mchezaji huyo.
Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kuonesha nia ya kutaka kuihama timu hiyo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa hafurahishwi na mambo yanavyokwenda ikiwamo uhakika wa nafasi katika kikosi cha kwanza.
Rodrygo 24, kwa sasa ana mkataba na Real Madrid ambao unafikia ukomo mwaka 2028 na kinachoonekana ni kama vile klabu hiyo inasita kumruhusu nyota huyo aondoke kwani hata habari hiyo ilivyojitokeza huko nyuma jaribio hilo halikufanikiwa.
Nyota huyo ambaye pia huichezea timu ya taifa ya Brazil, inaonekana safari hii amedhamiria kutafuta changamoto nje ya klabu hiyo licha ya mabosi wake kuwa wagumu kumruhusu.
Mashabiki na wachambuzi wengi wanamuona Rodrygo kuwa ni aina ya mchezaji mwenye kipaji ambacho kinakuwa bora na aliwahi kufananishwa na mastaa wengine wa Brazil, Neymar na Robinho.
Kimataifa Man United, Arsenal zamsaka Rodrygo
Man United, Arsenal zamsaka Rodrygo
Read also
