Na mwandishi wetu
Timu ya wanawake ya Simba Queens imetoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mahasimu wao Yanga Princess katika mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania iliyochezwa Jumapili Desemba 28, 2025 kwenye dimba la Azam Complex, Dar es Salaam.
Ushindi wa mechi hiyo ya Derby ya Wanawake umeifanya Simba Queens kuendelea kushika usukani wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 15 wakifuatiwa kwa karibu na timu ya wanawake ya JKT maarufu JKT Queens yenye pointi 13.
Mashujaa wa Simba Queens katika mechi hiyo walikuwa ni Jentrix Shikangwa na Aisha Mnuka ambao mabao yao yalitosha kuihakikishia heshima timu hiyo katika mechi hiyo.
Wakati mambo yakiwa si mazuri kwa timu ya wanaume ya Simba ambayo kwa miaka ya karibuni imekuwa ikinyanyaswa na timu ya wanaume ya Yanga, mambo ni tofauti kwa Simba Queens, kwao ni mwiko kugeuzwa wateja wa wanawake wenzao, Yanga Princess.
Soka Simba Queens yaitesa Yanga Princess
Simba Queens yaitesa Yanga Princess
Related posts
Read also
