Na mwandishi wetu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Kabudi amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Tafa Stars’ inayoshiriki Afcon 2025 kuhakikisha wanapata mafanikio zaidi ya yale ya CHAN.
Waziri Kabudi alitoa kauli hiyo leo Alhamisi Desemba 18, 2025 akiwa kwenye kambi ya timu hiyo jijini Cairo nchini Misri wakati akiwakabidhi wachezaji hao bendera ya taifa huku akiwataka wachezaji hao kuwa fahari ya Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kwenye vyanzo vya Shirikisho la Saoka Tanzania (TFF) Waziri Kabudi alifafanua kuwa katika CHAN, Stars iliishia hatua ya robo fainali hivyo ni muhimu kwenda mbele zaidi.
Michuano ya CHAN inayohusisha nchi za mataifa ya Afrika hushirikisha wachezaji wa ligi za ndani, ilifanyika hivi karibuni kwa pamoja katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.
Waziri Kabudi pia aliwaambia wachezaji wa Stars kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anawatakia kila la kheri na amemuhakikishia kuwa mafanikio ya CHAN hayakuwa madogo na huko Morocco wanawatakia mafanikio makubwa zaidi.
Katika fainali za Afcon 2025 zitakazofanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21, 2025, Stars imepangwa Kundi C na timu za Uganda, Tunisia na Nigeria na itacheza mechi yake ya kwanza Jumanne, Desemba 23 dhidi ya Nigeria.
Kimataifa Waziri ataka mafanikio zaidi Stars
Waziri ataka mafanikio zaidi Stars
Read also
