Na mwandishi wetu
Kamati iliyoundwa na Chama cha Waandishi wa Habrai za Michezo Tanzania (Taswa) kwa ajili ya kufanya maboresho ya uendesheji wa mfumo wa chama hicho imemaliza kazi yake.
Akizungumza Dar es Salaam Jumatano Desemba 17, 2025, mwenyekiti wa Taswa, Amir Mhando (pichani juu) amesema kamati hiyo chini ya mhariri mkongwe, Joseph Kulangwa iliandaa ripoti hiyo ikishirikiana na taaisis binafsi ya Frux.
Kwa mujibu wa Mhando, Frux walipewa jukumu la kuandaa mpango mkakati wa miaka mitano kuanzia 2025-2030 ili kukifanya chama hicho kijiendeshe kisasa zaidi kuendana na mabadiliko ya wakati.
Mhando alisema kamati ya utendaji ya Taswa itakutana hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa mkutano wa wadau wote muhimu ili kuzindua rasmi mpango huo na kuanza utekelezaji wake.
Alisema mapendekezo mengine ya maboresho ya mabadiliko ya kimfumo, yameingizwa kwenye rasimu ya mabadiliko ya katiba ya Taswa na baadaye yatapelekwa kwa wanachama kwa ajili ya kupata baraka zao.
Sports Mix Kamati Taswa yakamilisha kazi
Kamati Taswa yakamilisha kazi
Read also
