Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatarajia kufanya mkutano mkuu wa mwaka ambao utafanyika mjini Kahama mkoani Shinyanga, Februari 21 mwakani.
Taarifa ya TFF iliyopatikana Jumamosi Desemba 13, 2025 ilieleza kuwa mkutano huo wa kawaida wa 20 unafanyika kufuatia maamuzi ya kikao cha kamati ya utendaji ya shirikisho hilo kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Kikao cha kamati ya utendaji kilichoongozwa na Rais wa TFF, Walace Karia kilipitia na kujadili mambo mbalimbali ikiwamo taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Mkutano mkuu wa TFF utakaofanyika Kahama utakuwa wa kwanza tangu Karia achaguliwe tena kuliongoza shirikisho hilo baada ya uchaguzi uliofanyika Agosti mwaka huu na mgombea huyo kupata ushindi wa kishindo.
Uchaguzi huo hata hivyo ulipingwa na baadhi ya wadau wa soka ambao walipinga taratibu za uchaguzi na kitendo cha Karia kupitishwa kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo.
Baadhi ya wadau walipeleka suala hilo mahakamani wakidai uchaguzi huo ulikuwa batili wakitaka usitishwe na mchakato uanze upya ili watu wengine waruhusiwe kushindana na Karia kwenye sanduku la kura lakini mahakama ilizikataa hoja hizo na uchaguzi kufanyika kama kawaida.
Soka TFF kukutana Kahama
TFF kukutana Kahama
Read also
