Na mwandishi wetu
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Miguel Gamondi ametangaza wachezaji 28 wa timu hiyo ambao tayari wameelekea nchini Misri kujiandaa na fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025.
Wachezaji hao wametokana na mchujo uliotokana na orodha ya awali ya wachezaji zaidi ya 50 waliotajwa na kocha huyo ambaye alikiri kwamba kazi ya kuwachuja wachezaji hao haikuwa rahisi.
Idadi kamili ya wachezaji hao na timu wanazotoka katika mabano ni kama ifuatavyo, Yakoub Suleiman (Simba), Hussein Masalanga (Singida BS), Zubeir Foba (Azam FC) Shomari Kapombe (Simba), Mohamed Hussein (Yanga) na Lusajo Mwaikenda (Azam).
Wengine ni Bakari Mwamnyeto (Yanga) Nickson Kibabage (Singida BS), Alphonce Mabula (Shamakhi-Azerbaijan), Wilson Nangu (Simba), Novatus Dismas (Goztepe FC-Uturuki), Kelvin Nashon (Pamba Jiji), Ibrahim Abdullah (Yanga) Pascal Msindo (Azam FC) na Haji Mnoga (Salford City-Uingereza).
Wachezaji wengine ni Dickson Job (Yanga), Habib Idd (Singida BS), Tarryn Allarakhia (Rochdale AFC-Uingereza), Charles M’mombwa (Floriana FC-Malta), Yusuf Kagoma (Simba) na Feisal Salum (Azam FC).
Wengine ni Morrice Abraham (Simba) Abdul Suleiman (Azam FC), Idd Suleiman (Azam FC), Kibu Dennis (Simba), Mbwana Samatta (Le Havre AC-Ufaransa), Simon Msuva (Al Taraba-Iraq) na Kelvin John (Aalborg BK-Denmark).
Kimataifa Wachezaji Stars waelekea Misri
Wachezaji Stars waelekea Misri
Read also
