Rabat, Morocco
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limempa tuzo ya heshima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania, Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa wakati Tanzania ikiwa mwenyeji wa michuano ya CHAN 2024.
Tanzania ilikuwa mwenyeji wa michuano ya CHAN ambayo hushirikisha wachezaji wa ligi za ndani wa timu za mataifa ya Afrika, michuano ambayo wenyeji pia walikuwa Kenya na Uganda.
Katika tuzo hiyo CAF pia imethamini michango ya marais wa Kenya, William Ruto na Yoweri Museveni wa Uganda ambao kama ilivyo kwa Rais Samia nao wamepewa tuzo hiyo.
Katika hafla ya utoaji wa tuzo hiyo, tuzo ya Rais Samia ilipokewa kwa niaba yake na katibu mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa.
Katika salamu zake, CAF imesema kuwa imetoa tuzo hiyo kwa viongozi wa Tanzania, Kenya na Uganda kwa lengo la kuthamini maandalizi bora ya michuano hiyo katika nchi hizo tatu za Afrika Mashariki.
Tanzania, Kenya na Uganda pia ndizo nchi zinazotarajia kuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2027.
Kimataifa CAF yampa tuzo Rais Samia
CAF yampa tuzo Rais Samia
Read also
